BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Jay C Production : Mpango wetu ni kuona tasnia ya filamu ya Burundi inazidi kuendelea na kufika mbali

Nyumba ya utengenezaji wa filamu nchini Burundi JAY C PRODUCTION ni company kubwa ambayo inazidi kusaidia wasanii wote kwa ujumla kuanzia kwa waimbaji wa nyimbo hadi kwa waigizaji wa filamu nchini Burundi na ni nyumba pia yenye kueneza vifao vizuri vya kazi kama vinavyo itajika kwenye kazi za video na pia company hio imeshatumika na wasanii wengi  sana ikiwemo ma star wa Buja fleva pia na wa star wa buja Movie na kazi zao kuzidi kuonekana kwenye Channel yao zenye mafunzo na kuburudisha.

Basi baada yakusikia kwamba kuna promo inayo fanyika tumewezaa kuwatembelea nakuuliza nini malengo yao basi majibu yamtoka kwa manager wa JAY C PRODUCTION:

MANAGER:

“Kwanza moja tu nashukuru sana kuona filamu ya Burundi inazidi kusonga mbele siku kwa siku na waigizaji kuanza kujielewa  pia nikipenda kuongeleya company yetu ya JAY C PRODUCTION na weza sema kwamba kwa upande wetu sisi tunayo malengo makubwa sana yakuinuwa tasnia ya filamu Burundi ikiwa kwamba wasanii watajielewa vizuri nakujuwa nini wanacho kifanya kwa hiyo inatubidi sote kwa pamoja tuweke nguvu ili kuakikisha filamu ya Burundi inainuka na sisi pendeleo letu sio tu kwa waigizaji bali pia na kwa wasanii waimba music ila tunazidi kushukuru maana tuna vijana wanaozidi kufanya vizuri siku kwa siku na kazi zao kuanza kupendwa nje ya nchi basi na kwa fursa hiyo tumeweza kutowa msaada wa promo kwa wasanii wote wenye kufanya kazi za sanaa kwa upande wa music na filamu pia na wanakaribishwa kwenye studio yetu ya Jay C Production kwa maelezo mengi zaidi yote ni njia ya kuweza kuwasaidia waweze kufikia ndoto zao ,maana kama ilivyo ndoto yetu nikuona vijana wetu wanaanza kujulikana nje ya nchi kama ilivyo wasanii wengine wa nchi jirani tunavyo wafaamu apa Burundi”.

Alimaliza Manager wa JAYC PRO

Kweli Burundi waigizaji wengi wa filamu walikuwa wakikosa fursa ya kwenda kushoot na vifao vizuri vyenye kuleta kazi nzuri ,maana mwanzo wasanii walikuwa wakifanya na camera ndogo ata mic boom walikuwa hawana nakusababisha filamu zao kutoka na Quality mbaya pia na sauti mbaya ila kwa sasa tunaanza kuona mabadiliko yote inatokana na ma company kuanza kujitokeza kwa wingi,kweli pole pole ndo mwendo lazima watafikia.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 717