homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Jacklus, Msanii wa Filamu nchini Burundi na ujio wa filamu yake mpya “Mitiani”.

Jacklus muigizaji wa Filamu za kiswahili nchini Burundi kwa sasa amesema kuwa anakuja kitofauti sana kwenye iyi game na amejifunza mengi sana kupitia kazi yake ya filamu kutokana na sehemu kubwa anayoipenda sana kwenye game kuwa Director mkubwa.

Basi alivyoitwa kwenye Tv ya Indundi basi katika maojiano amesema kuwa :

“Mimi kwa sasa napenda kuwa Director japo kuwa nacheza ila iyo sio ndoto yangu ila naamini ipo siku itatimia tu, na kutokana na filamu yangu ambayo siku za usoni nitaachia inayo kwenda kwa jina la MITIANI. Kweli ni movie kubwa na yenye utofauti kabisa mkubwa sana pia kwa maandalizi ninayo yafanya naamini tu itapokelewa vizuri sana na kwenye iyo iyo movie nina surprise nyingi sana kwa mashabiki wangu, wajiandae tu japo kuwa nimekutana na changamoto nyingi sana ila naamini mambo yatakuwa mazuri sana”.  Aliongea Jacluks.

Basi Jacklus ni msanii anaejituma kwa kazi na ameweza kuishukuru sana Indundi Tv kwa kuleta kipindi chakusaidia waigizaji wa filamu Burundi pia ikiwa na wewe unazo ndoto za kuwa muigizaji maarufu Indundi inasaidia.

 

What's your reaction?

Related Posts

1 of 688