BurundihomepageIndundi CinemaMoviesswahili

Ahishakiye Fanny : “Sina ndoto ya kuwa kama Irene Uwoya maana nami nina ndoto yangu”

Muigizaji wa filamu nchini Burundi Ahishakiye Fanny maarufu kama Fanny amefunguka na kusema kwamba mimi sina ndoto kama ya mwenzangu ila nina ndoto yakuwa kama mimi. Ikumbukwe kuwa Fanny ameonekana kwenye Shortfilm iitwayo THE SHOCK na ameonesha uwezo mkubwa sana wa kuigiza, na Filamu hio imependwa na watu kibao kabisa tena kwa hali ya juu.

Basi alipo ulizwa nini anacho fikiria na anatamani awe kama muigizaji gani amesema Fanny:

“Mimi sina ndoto yakuwa kama msanii yeyote wa kike mfano kama Irene Uwoya ao Aunty Ezekiel unajuwa ili wao wajenge Brand zao sijuwi wamefanya nini ao ni mangapi walio vumilia, kwa hio ni ngumu kuwa kama wao ila naamini mimi nitakuwa kama mimi, na baada yakutengeneza Filamu ya THE SHOCK nimeona utofauti mkubwa sana wamapokezi ya watu nikaona kwamba naamini ipo siku nitakuja kufikia malengo yangu maana nimeona watu wameipenda sana niseme tu kwamba naamini nitafikia malengo yangu ya kuinuwa jina langu na sio apa Burundi tu maana nina ndoto yakufika kimataifa kwa hii mashabiki wangu wakae tayari kwa sasa nakuja kitofauti pia naamini nitafika tu, na kwasasa niko naandaa kazi kubwa tena nzuri sana mda sio mrefu wataniona”. Alimaliza Fanny.

Burundi inaweza kuwa kama Tanzania na ikazidi maana Tanzania waigizaji wakike ni wengi wanaojituma tunaamini Burundi kwa kweli italeta mabadiriko makubwa mda sio mrefu.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 717