homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Harerimana Hamu : “Mimi ni actress anaejielewa na sipo tayari kufanya filamu za kitoto”

Katika Tasnia ya Filamu nchini Burundi kwa upande wa filamu za kiswahili ni moja ya secta iliyo kosa kabisa waigizaji wa kike ,ila Hamu ni mmoja kati ya wa actress wanaoigiza filamu za kiswahili vizuri na ameweza kushiriki filamu nyingi ikiwemo wasanii wakubwa wa nchi ya Tanzania na amezidi kuonesha uwezo mkubwa sana katika uigizaji wake, pia aliweza kushiriki kwenye filamu ambayo Soon itafanyiwa uzinduzi na ameshiriki kama Principal Actress.

Basi tulipo muuliza kwanini amekaa kimya mda mrefu amejibu Hamu:

“Mimi sipo kimya ila nakaa nakufikiria kazi kubwa maana mimi sio msanii wakutafuta tu jina bila kutazama ni njia gani ambayo ipo sahihi kwangu, kweli nimefanya Filamu za kutosha sana na nimeshiriki na wasanii wakubwa kuanza apa hadi nje ya nchi ila kuna kitu najifunza mda kwa mda ikiwa nitabaki nashiriki kwenye kazi ambazo hazina maana nitajikuta naaribu jina ambalo nimejenga kwa mda mrefu sana, kweli tunajitaidi sana apa nyumbani ila naomba sana waigizaji wajitaidi waache mambo ya kuteng’neza filamu za kitoto tukae chini tufikirie makubwa zaidi maana wenzetu kama wameendelea haikuwa kwa ajili ya jina bali ni ajili ya kazi walizo ziteng’neza. Niwajulishe tu washabiki kwamba mimi Hamu bado nipo najuwa wapo na Hamu yangu yakuniona kwenye Filamu kwa iyo wasubiri mda sio mrefu wataona ninavyo kuja tena na utofauti mkubwa zaidi”. Alimaliza ivo Hamu.

Ikiwa wanawake wa Burundi wataelewa kuwa wanao mchango mkubwa ndani ya filamu ninayo imani kwamba wanamchango pia wakuleta mabadiliko maana filamu nayo inaitaji wanawake warembo.

Tunawatakalia mafanikio mema ndani ya sanaa ya maigizo.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 688