East Africa NewshomepageIndundi CinemaMoviesswahiliTanzania

Breaking news : Baba Kanumba afariki dunia

Baba mzazi wa Marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amefariki Machi 8, 2020, saa nne asubuhi akiwa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Mdogo wake Kanumba, Mjanaeli Kanumba amethibitisha. Aliugua kwa muda mrefu

“Kweli Baba ameuguwa kwa mda mrefu sana kabisa na tulikuwa tukifatilia hali yake kwa sana ,na mzee amekuwa tayari anasumbuliwa na Magonjwa mengi sana ila inatuumiza sana kama wanafamilia kumpoteza mzee wetu ,maana ndie alikuwa mshauri wetu kwa upande mkubwa. Basi Mungu alimpenda zaidi yetu ,tunawaombea wote na kaka Marehemu Steven Charles Kanumba”

Ikumbukwe kwamba kuna kesi kubwa ambayo ilioleta matatizo baina ya mama Kanumba na Marehemu baba Kanumba kwa ajili ya pesa ambazo zinazo tolewa kwa ajili ya kazi ya Marehemu Kanumba na makampuni ambazo alikuwa nazo mkataba ,na pesa izo kabisa zinazidi kuletea fujo baada ya mama Kanumba kuonekana kutumia mwenyewe pesa ya mwanae bila kumpa baba Kanumba.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 690