homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Mdogo wake marehemu Steven Kanumba kalazwa hospitali Muhimbili

Mdogo wake marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco yupo hoi kitandani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la mwili kufa ganzi.

Seth amepatwa na tatizo hilo ambapo mwili wake kuanzia sehemu ya kiunoni hadi miguuni, viungo vyote havifanyi kazi.

“Nina kama wiki ya pili sasa tangu niletwe hapa Muhimbili, mwili haufanyi kazi kuanzia kiunoni hadi miguuni. Kabla ya hapo hali hii ilinijia ghafla tu. Nimefanyiwa vipimo na madaktari wameniambia natakiwa kufanyiwa upasuaji hivyo nasubiria,” Alisema Seth.

Enzi za uhai wa Kanumba ukimtoa Lulu ambaye alikuwa ni mpenzi, Seth alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anajua siri nyingi za Kanumba kwani ndiye alikuwa ndugu yake walioshibana.

Mungu akusaidie Seth uweze kurudi katika hali yako ya kawaida.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 688