homepageCECAFA Challenge cupIndundi CinemaMoviesswahili

Msanii afaamikae kwa jina la EBITOKE akitowa ukweli wa rohoni

Komediani Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ utacheka, maana mwenyewe ameapa kumzalia mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa kiume wa Bongo Movies, Yusuf Mlela. Ebitoke amelisema kuwa, anawashangaa wanaomponda kwamba haendani na Mlela na wanakaa wanamuongelea kwenye mitandao mda kwa mda.

Lakini ukweli ni kwamba lazima amzalie ndiyo watafunga midomo. “Mimi ninajiuliza, kwa nini watu wanachonga sana kuhusu uhusiano wetu? Sasa hivi najipanga kumpa Mlela zawadi ya mtoto ndiyo watu watafunga midomo”. Alisema Ebitoke ambae kapo yake na Mlela ni gumzo Bongo

Ikumbukwe kuwa ni baada ya Ebitoke kutoka kwenye Company ya Timamu Tv ambao imekuwa ikimtengenezea jina Ebitoke hadi kujulikana na kwa sasa kujipatia umaarufu mkubwa.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 688