homepageIndundi CinemaMoviesswahili

Zamda anajikubali nakusema kwamba yeye ni Actress mwenye uwezo mkubwa

Muigizaji wa Filamu nchini Burundi kwa jina la Iradukunda Zamda maarufu kama Ange apo ni baada yakufanya movie iitwayo USALITI nakuonesha uwezo mkubwa sana kwenye Filamu iyo hadi baada ya kutowa Trailer ya Filamu hio nakuweza kujipatishia washabiki wengi sana nakuweza kukubalika. Basi hapo ni baada ya maojiano yake na Indundi Tv mwana dada huyo amefunguka mambo mengi sana uku akisema :

“Kusema ukweli kwa sasa nimeona jina limepanda sana kupita kiasi na ninajiamini sana sasa maana nikama ndoto yangu inakwenda kutimia siku ambayo nilipenda Filamu, nakujiingiza kuigiza imekuwa tu kama mtani, hapo nilikutana na rafiki yangu akienda zoezini namimi nikasema twende nilipo fika nikajikuta pia na mimi naanza kuigiza hadi sasa nikachaguliwa kuwa Actress principal kwenye hiyo Filamu, niseme tu kwamba iyo Filamu imenionesha ni jinsi gani jina langu litakavyo kuwa kubwa. Pia ni seme na najikubali sana na mimi ni actress mwenye uwezo mkubwa sana nchini Burundi na sijaona wakunifata, na kama yupo basi ajitokeze nayeye kwenye game ili nione, na baada ya hii Filamu kuna kuja nyingine kubwa kuliko hii, kaeni mkao wa kula.” Alimaliza Zamda

Hapo ni baada ya kufanya maojiano na mrembo huyo na kuonesha kabisa uwezo mkubwa wa usanii wake, kweli Filamu inaomba ubunifu na mtazamo wa sasa.

What's your reaction?

Related Posts

1 of 688